Jina la kiungo fundi wa KMC Awesu Ally Awesu ni miongoni mwa wachezaji wa ndani waliopendekezwa kusajiliwa na mabingwa wa kihistoria Tanzania, Yanga, imefahamika
Awesu ni miongoni mwa wachezaji wa ndani ambao wana nafasi kubwa ya kutua kuimarisha kikosi cha Yanga kuelekea msimu ujao
Kiungo huyo mahiri mwenye uwezo mkubwa kumiliki dimba la kati, pengine ndiye 'rasta' anayetajwa tajwa na msemaji wa Yanga Ali Kamwe
Awesu atakuwa mchezaji huru pale msimu utakapofika mwisho kwani mkataba wake na KMC utakuwa umefika tamati
Katika moja ya mahojiano na Kamwe, alisema kuwa umefika wakati kwa Awesu kucheza timu kubwa inayoshinda makombe
Awesu kutoka visiwani Zanzibar, amewahi kuzitumikia Kager Sugar na Azam Fc kwa nyakati tofauti kabla ya kutua KMC
ADVERTISE HERE