Kocha wa zamani wa Yanga Mohammed Nasreddine Nabi amewapongeza waajiri wake hao wa zamani kwa kutwaa ubingwa wa ligi kuu kwa msimu wa tatu mfululizo
Nabi ambaye aliiongoza Yanga kutwaa mataji ya ligi kuu 2021/22 na 2022/23 amesema Yanga ilistahili kutwaa taji hilo kwa mara nyingine
"Hongera Yanga kwa kuwa mabingwa wa ligi kuu ya Tanzania, ni ubingwa mliostahili," aliandika Nabi katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii
Nabi aliondoka Yanga msimu uliopita baada ya kuwaongoza Wananchi kutwaa mataji yote ya ndani pamoja na kucheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika
Alijunga na klabu ya AS Far Rabat ya Morocco akikaribia kuipa timu hiyo ubingwa wa ligi kuu ya Morocco kwa msimu wa pili mfululizo
ADVERTISE HERE