Msafara wa wachezaji 20 pamoja na viongozi 11 wakijumuisha benchi la ufundi, unaelekea mkoani Kigoma kwa ajili ya mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mashujaa Fc utakaopigwa kesho Jumapili, May 05 katika uwanja wa Lake Tanganyika
Yanga inakwenda Kigoma kwa usafiri wa ndege ambapo jioni ya leo wanatarajiwa kufanya mazoezi ya mwisho kunako dimba la Lake Tanganyika
Yanga iko kwenye mkakati wa kukamilisha hesabu za ubingwa hivyo ni mchezo ambao Wananchi wanazihitaji alama zote tatu
Wakiwa kileleni mwa msimamo wa ligi na alama 62, Yanga inahitaji alama nyingine 11 ili kutetea ubingwa kwa msimu wa tatu mfululizo
Mechi za mwishoni mwa msimu mara nyingi huwa sio nyepesi lakini ili uwe bingwa lazima upate ushindi katika mechi ngumu
Mashujaa Fc haiko salama katika msimamo wa ligi, inapigania kujinusuru na hatari ya kurudi Championship hivyo ni wazi watawapa Wananchi mechi ngumu