No One Can Stop Reggae - Arafat

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
3 May 2024
No One Can Stop Reggae - Arafat

Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji amewataka Wanachama na Mashabiki kulipia kadi za uanachama wao kwani wao ni sehemu ya familia ya Yanga

Arafat amesema mafanikio ambayo Yanga inapata chini ya uongozi wao, yanatokana na sapoti na ushirikiano kutoka kwa kila Mwananchi

Licha ya uongozi wa Yanga chini ya Rais Injinia Hersi Said kupewa kila aina ya majina wakati wanaingia, lakini walisimama imara, wakafanya kazi na leo hawahitaji kuzungumza sana kwa sababu mafanikio yanaonekana

Kupitia ukurasa wake wa mtandao ya kijamii, Arafat ameandika ujumbe huu;

"Wastani wa umri ni wa kati, hadhi ni ya Ujana na sifa tulipewa ni WAHUNI, hupaswi kukataa sifa ambayo watu wamekupa na hupaswi kupinga pale ambapo watu wamekuweka, maneno yawe kidogo sana, mdomo mmoja na masikio mawili ili uzungumze kidogo na kusikia sana.

Kwenye umri wa UJANA tumeishi na misemo ya Wahenga kuwa Ukubwa ni jalala, haikuwa ukubwa wa umri bali ndoto ndani ya hii klabu kubwa nchini, kimalengo bado hatujafanikiwa na safari bado ni ndefu sana huku lengo ni kuishika Afrika siku moja.

Kwenye umri wetu huu tunaendelea kujifunza, kusaka maarifa, kukubali kukosolewa na mawe yote tutajengea, maneno yote yatatujenga ila kikubwa WANANCHI tuwe nyuma ya klabu yetu, hakuna mshindi zaidi ya Yanga Imara iliyoungana, una wazo wasilisha, una kero iseme tena kwa sauti ya juu na ukichukizwa ongea usikike hii ni timu yetu sote.

Ninachoweza kuwaomba WANANCHI lipieni kadi za Uanachama muwe sehemu ya hii familia kubwa, huanza na ndoto kwakuwa sisi hatupo hapa milele, Kiongozi ajae ni wewe kuwa sehemu ya hii familia, changia klabu yako kwa kununua bidhaa na kulipia kadi pamoja na kujiunga na hii familia, tufanye kwa ajili ya klabu yetu.

“No One Can Stop Reggae, Even the Voiceless..”

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’