Mwezi April ulikuwa bora sana kwa mshambuliaji Joseph Guede aliyetua kwa Wananchi katika usajili wa dirisha dogo Januari 2024
Mabao yake manne aliyofunga katika mwezi huo yanamuweka katika nafasi nzuri ya kubeba tuzo mbili; tuzo ya mwezi ya Ligi Kuu na hata tuzo ya mwezi ya Yanga
Leo Yanga inashuka tena uwanja wa Azam Complex kuikabili Tabora United katika mchezo wa robo fainali kombe la Shirikisho la CRBD. Mtanange huo unatarajiwa kupigwa kuanzia saa 2:30 usiku
Guede ambaye pia ana bao moja la ligi ya mabingwa na mabao mawili ya kombe la FA, bila shaka atakuwa sehemu ya kikosi cha Wananchi kitakachoshuka dimbani leo
Hii itakuwa nafasi nyingine kwake kuendelea kudhihirisha ubora wake na kuwazima wale waliokosoa usajili wake na Yanga
Idadi ya mabao aliyoifungia Yanga katika mashindano yote mpaka sasa ni saba