Mikiki mikiki ya ligi kuu ya NBC inaendelea leo ambapo mabingwa watetezi Yanga watakuwa nyumbani uwanja wa Azam Complex kuikabili Coastal Union
Baada ya kulazimishwa suluhu katika mchezo uliopita, leo wananchi wataingia dimba la Azam Complex wakiwa na dhamira moja tu, ushindi
Katika Mkutano na Wanahabari jana, Mkufunzi wa Yanga Miguel Gamondi alisema anahitaji kuona vijana wake leo wakiwa katika ubora mkubwa ili kushinda mchezo huo
Coastal Union wamekuwa bora msimu huu wakishika nafasi ya nne katika msimamo wa ligi nao wakiwania tiketi ya kushiriki Kimataifa msimu ujao
Habari njema ni kuwa hali ya hewa ni nzuri, hakuna dalili kubwa ya mvua pengine leo soka safi litashuhudiwa uwanja wa Azam Complex
Kama Yanga itashinda mchezo huo itaendelea kusogelea ubingwa wa 30 msimu huu
Mchezo huo utapigwa kuanzia saa 12 jioni