Lwandamina kurejea ZESCO mwishoni mwa msimu

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
10 Apr 2018
Lwandamina kurejea ZESCO mwishoni mwa msimu
Mkataba wa kocha Mkuu wa Yanga George Lwandamina unamaliza mwishoni mwa mwezi wa tano, siku chache baada ya kumalizika ligi kuu ya Vodacom msimu wa 2017/18.

Kulingana na vyombo vya habari nchini Zambia kuna kila dalili Lwandamina pamoja na msaidizi wake Noel Mwandila watarejea katika klabu yao ya zamani ZESCO United.



Kulingana na mtandao wa ZambiaFootball, ZESCO imeshamalizana na kocha huyo aliyewapa mataji ya ligi kuu ya Zambia kwa misimu miwili mfululizo.

Mtandao huo umekwenda mbali zaidi kwa kudai kwamba kwa mujibu wa vyanzo vyake vya habari, kocha huyo tayari ameshasaini mkataba wa awali na anatarajiwa kutambulishwa katika klabu hiyo leo.

Habari ya Lwandamina kurejea ZESCO iliripotiwa sana na vyombo vya habari nchini Zambia mwezi uliopita.

Alipoulizwa kuhusu taarifa hiyo, Katibu Mkuu wa Yanga Charles Mkwasa alisema Lwandamina bado ana mkataba wa kuitumikia Yanga hadi mwishoni mwa msimu baada ya hapo ni yeye mwenyewe atakayeamua abaki Yanga au akafanye kazi mahali pengine.

ZESCO imetinga hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika na tangu kujiuzulu kwa aliyekuwa kocha wake Tenant Tembo timu hiyo haijamtangaza kocha mwingine hivyo kuashiria kwamba huenda Lwandamina akawa njiani kurejea katika klabu hiyo.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
1h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
16h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
20h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1d ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’