Maxi, Aziz Ki kusaka rekodi dhidi ya Simba

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
20 Apr 2024
Maxi, Aziz Ki kusaka rekodi dhidi ya Simba

Katika mechi iliyopita, Maxi Nzengeli alikuwa na nafasi ya kuifikia rekodi ya Mzee Abdallah Kibadeni ambaye ni mchezaji pekee aliyewahi kufunga mabao matatu 'hat-trik' katika mechi ya derby ya Kariakoo

Akiwa tayari amepachika mabao mawili, wengi walitamani Maxi apige mkwaju wa penati ambayo Yanga waliipata katika dakika za majeruhi

Lakini Pacome Zouzoua akapewa jukumu la kupiga penati hiyo na kukamilisha utatu wa MAP kufunga katika mchezo ambao Yanga iliibuka na ushindi wa mabao 5-1

Bila shaka leo tena Maxi atakuwepo uwanjani katika mchezo utakaopigwa saa 11 jioni, Yanga ikiwa mwenyeji

Kama atafunga, Maxi ataingia katika rekodi ya wachezaji waliofunga mabao matatu katika mechi tofauti za derby

Mcongomani Fiston Mayele aliyeitumikia Yanga kwa misimu miwili ni miongoni mwa wachezaji walioifunga Simba mara tatu katika misimu ya karibuni

Stephane Aziz Ki ana mabao mawili kama ilivyo kwa Maxi, nae ana nafasi ya kuongeza idadi yake ya mabao

Wakati yuko Asec Mimosas Aziz Ki pia aliifunga Simba mabao mawili na jumla kuwa amewafunga mabao manne

Akiwa kinara wa mabao ligi kuu ya NBC (14), Aziz Ki leo huenda ataongeza namba ya mabao yake na kujiweka katika nafasi nzuri ya kuibuka mfungaji bora

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
8h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
8h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
12h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
17h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
17h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’