Gamondi asifu morali ya wachezaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Apr 2024
Gamondi asifu morali ya wachezaji Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga, Miguel Gamondi, amewasifu wachezaji wake wanavyopambana mazoezini ili kuhakikisha wanakuwa imara na tayari kupata ushindi katika michezo yao iliyoko mbele

Gamondi amesema hata katika michezo ambayo hawakupata ushindi, nyota wake hupambana na kinachowazuia ni suala la bahati

"Ukiangalia wachezaji wanavyocheza unaona kabisa wanavyojitoa kwa ajili ya timu yao, tunapokosa ushindi tunakuwa tumekosa bahati tu lakini wachezaji wanakuwa wamefanya kazi yao kwa uhakika," alisema

Gamondi amebainisha kuwa kila wanapokuwa kwenye uwanja wa mazoezi wanatumia muda mwingi kusisitiza kuhusu hali ya upambanaji ili kupata matokeo mazuri kwa ajili ya kutimiza malengo

Akizungumzia mchezo unaofuata ligi kuu dhidi ya Singida FG ambao utapigwa kesho Jumapili katika uwanja wa CCM Kirumba, Gamondi amesema hatarajii mechi hiyo kuwa nyepesi

"Tunatambua kila timu ipo katika mashindano hivyo imejiandaa vizuri, utakuwa mchezo mgumu lakini tunahitaji ushindi kuhakikisha tunatetea taji la Ligi Kuu Tanzania Bara," Gamondi alisema

Katika msimamo wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Yanga inaongoza ikiwa na pointi 52 zilizovuna katika michezo 20 wakati Singida Fountain Gate iko nafasi ya saba, imejikusanyia pointi 24 baada ya kushuka dimbani mara 21. Yanga ndio mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara na mashindano ya Kombe la FA

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
10h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
15h ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
19h ago
READ MORE β†’
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
Yanga mpya kuanza na Mashujaa Fc, hivi hapa viingilio
20h ago
READ MORE β†’
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
Hersi akimpata huyu wamekwisha!
20h ago
READ MORE β†’
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
Droo ya makundi CAF ni Jumatano
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
Yanga yarejea Dar, kujipanga dhidi ya Mashujaa Fc
1d ago
READ MORE β†’
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
Behlulovic anasubiri simu ya Injinia Hersi
1d ago
READ MORE β†’