Yanga imetinga robo fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho la CRDB baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Dodoma Jiji katika mchezo uliopigwa uwanja wa Jamhuri mkoani Dodoma
Yanga ilipata bao la kuongoza mapema tu kwenyee dakika ya 3 baada ya Emmanuel Martin kujifunga katika jitihada za kuokoa krosi ya Augustine Okrah
Bao hilo lilidumu mpaka wakati wa mapumziko. Kipindi cha pili Yanga ilirejea na kasi kubwa lakini kukosekana kwa umakini kuliwanyima nafasi ya kufunga bao la pili mapema
Dodoma Jiji walipata mkwaju wa penati lakini Iddi Kipagwile alikosa mkwaju huo
Clement Mzize aliihakikishia Yanga ushindi muhimu katika dakika 66 akifunga bao la pili
Ulikuwa mchezo mgumu Dodoma Jiji walitoa upinzani mkali lakini ubora wa Yanga uliamua matokeo ya mchezo huo