Aziz Ki ameongeza mzuka wa kikosi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
5 Apr 2024
Aziz Ki ameongeza mzuka wa kikosi

Ukisikia mechi kubwa, mechi ambayo wachezaji wanaitaka basi mechi ya leo Yanga ikichuana na Mamelodi huko Afrika Kusini ni moja ya mechi hizo

Ukiona mpaka wachezaji wanaahidi kutoa zawadi kwa wenzao kama watafanya vizuri basi hiyo inaonyesha ni kwa kiasi gani wamedhamiria kushinda na kuandika historia ya kutinga nusu fainali

Kuna bonas ziliahidiwa na uongozi wa Yanga, GSM bila kusahau goli la Mama. Nyota Stephane Aziz Ki yeye ameahidi kutoa Tsh Milioni 1 kwa kila mchezaji atakayefunga bao katika mchezo huo leo

Aziz Ki hakuishia hapo, pia ameahidi kutoa Tsh Milioni 1 kwa safu ya ulinzi na golikipa kwa pamoja kama watahakikisha hakuna bao Mamelodi wanafunga leo

Hii ni mechi ya wachezaji hii ni mechi ambayo wachezaji wa Yanga wanaitaka heshima katika soka la Afrika

Baada ya msimu uliopita kucheza fainali ya kombe la Shirikisho na kukosa taji hilo kwa kanuni ya bao la ugenini, msimu huu wanataka kusahihisha makosa kupitia ligi ya mabingwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
4h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’