Gamondi apongeza wachezaji Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
31 Mar 2024
Gamondi apongeza wachezaji Yanga

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amewapongeza wachezaji wake licha ya kukosa ushindi dhidi ya Mamelodi Sundowns katika mchezo wa mkondo wa kwanza robo fainali ligi ya mabingwa uliomalizika kwa matokeo ya 0-0

Gamondi amesema wachezaji wake walitekeleza vyema mpango wa kimbinu walioingia nao katika mchezo huo na walikuwa na nafasi nzuri zaidi ya kushinda

"Nawapongeza wachezaji wangu haikuwa mechi rahisi hata kidogo. Kwa maoni yangu Mamelodi Sundowns ndio klabu bora barani Afrika kwa sasa"

"Ni lazima tuwaheshimu kwa ubora walionao na ndio maana hata mkakati wetu wa mechi ulibadilika"

"Tulikuwa na nafasi nzuri zaidi ya kufunga lakini hatukutimia vyema nafasi, jambo muhimu hatukuruhusu kufungwa bao nyumbani"

"Tutakwenda Afrika Kusini kupambana kusaka nafasi ya kuingia hatua ya nusu fainali," alisema Gamondi

Katika mchezo huo Yanga ilipiga mashuti saba huku manne yakilenga lango (on target). Kulikuwa nafasi mbili bora zaidi ambazo kama Kennedy Musonda na Clement Mzize wangeongeza umakini, wangeifungia Yanga

Mamelodi Sundowns walipiga mashuti 10 lakini ni mawili tu yaliyokuwa 'on target'

Katika mechi nne za robo fainali ni mechi moja tu ambayo Al Ahly waliichapa Simba bao 1-0, mechi nyingine tatu zimemalizika kwa matokeo ya 0-0

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’