Bacca uhakika kuikabili Mamelodi

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Mar 2024
Bacca uhakika kuikabili Mamelodi

Peter Shalulile ndiye mshambuliaji hatari wa Mamelodi Sundowns akiwa amefunga mabao mawili katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa msimu huu

Ni miongoni mwa wachezaji ambao Yanga lazima iwe na tahadhari nae katika mchezo wa robo fainali CAF CL utakaopigwa Jumamosi, March 30

Habari njema ni kuwa Yanga itaingia katika mchezo huo ikiwa nyota wake wote katika safu ya ulinzi akiwemo Ibrahim Hamad 'Bacca'

Kumekuwa na upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii kuwa Bacca hatacheza mchezo huo kutokana na kadi mbili za njano alizoonyeshwa katika michezo dhidi ya Al Ahly na CR Belouizdad

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amewahakikishia Wananchi kuwa Bacca atakuwepo

"Kwanza lazima ifahamike kanuni za michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu ni tofauti na kanuni zilizotumika msimu uliopita"

"Bacca alipata kadi tatu za njano katika hatua za awali akakosa mchezo dhidi ya Medeama Fc. Baada ya mchezo huo akapata kadi mbili za njano katika michezo iliyofuata dhidi ya Ahly na Belouizdad"

"Hivyo atakuwa sehemu ya kikosi kitakachoikabili Mamelodi Sundowns, " alisema Kamwe

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
1h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
1h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
12h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
15h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
19h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
22h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’