Wachezaji Pacome Zouzoua, Kennedy Musonda, Djigui Diarra na Stephane Aziz Ki jana walikamilisha mechi za Kimataifa za kirafiki katika timu zao za Taifa wakitarajiwa kuwasili nchini leo
Habari njema kwa Wananchi ni kuwa wachezaji wote wanarejea wakiwa fit hakuna aliyepata majeraha katika timu ya Taifa
Nahodha Bakari Mwamnyeto na Aboutwalib Mshery ambao walikuwa na kikosi cha Stars wao tayari wamerejea
Yanga ina siku tatu za kukamilisha maandalizi yake kabla ya kuikabili Mamelodi Sundowns Jumamosi March 30 katika mchezo ambao Wananchi wanahitaji ushindi ili kujiweka katika nafasi nzuri ya kutinga nusu fainali
ADVERTISE HERE