Buswita kukabidhiwa mikoba ya Chirwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Apr 2018
Buswita kukabidhiwa mikoba ya Chirwa
Kiungo mshambuliaji Pius Buswita huenda akaongoza safu ya ushambuliaji ya Yanga kwenye mchezo wa kesho dhidi ya Welayta Dicha.

Yanga imerejea mapema leo kutoka Morogoro ilikokuwa imeweka kambi ya siku tatu kujiandaa na mchezo wa kwanza wa kusaka tiketi ya kufuzu kwa hatua ya makundi kombe la Shirikisho barani Afrika.

Wakati Amissi Tambwe akiondolewe kabisa kikosini, Donald Ngoma ana uwezekano mdogo wa kucheza mchezo huo (50/50).

Ikumbukwe Obrey Chirwa hatacheza mchezo huo kwa kuwa anatumikia adhabu ya kadi mbili za njano sambamba na Kelvin Yondani, Said Juma na Papi Tshishimbi.

Kwa hali hiyo kocha George Lwandamina atalazimika kumtumia Buswita kama mshambuliaji na haitakuwa mara ya kwanza kwa kiungo huyo kucheza nafasi hiyo msimu huu.

Kocha Msaidizi wa Yanga Shedrack Nsajigwa amesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda mchezo huo licha ya kukosekana wachezaji wake muhimu.

Msimu huu Yanga imekuwa ikikumbana na changamoto za hapa na pale katika kikosi chake lakini jambo jema ni kwamba imekuwa ikifanya vizuri.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’