Serikali yatahadharisha sapoti kwa wageni CAF CL

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Mar 2024
Serikali yatahadharisha sapoti kwa wageni CAF CL

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Damas Ndumbaro amesema Serikali itakutana na Shirikisho la Soka nchini na klabu za Simba na Yanga ili kuona inatoa mchango gani kuhakikisha timu hizo zinafanya vizuri robo fainali na kusonga mbele.

Waziri Ndumbaro amesema pamoja na mambo mengine, amewataka mashabiki kuacha kuwapokea mashabiki na wafahamu mechi hizi za robo fainali ni kufa na kupona na kinachotakiwa ni kuhakikisha timu zetu zinashinda.

Amesema Serikali itakula sahani moja na mashabiki ambao wataenda kupokea wageni uwanja wa ndege na kuwasapoti.

"Wiki iliyopita tulitoa tamko, Serikali tunataka kukaa na Simba, Yanga na TFF, ili watuambie kama serikali, tunahitaji kutoa mchango gani ili timu kushinda robo fainali na ziingie nusu fainali. Tunaweza kukutana Jumanne wiki ijayo ili kupanga mikakati."

"Watanzania niwaombe sana najua kuna utani wa jadi, lakini kwenye mechi hizi za robo fainali ni mechi za kufa na kupona, hatutegemei kuona Mtanzania yeyote akienda kupokea wageni uwanja wa ndege, ama kuvaa jezi za timu za wageni."

"Sisi kama Serikali hatutawaachia hili TFF wala Simba na Yanga, kwa hiyo tukihangaika na mtu ambaye tutaona ni msaliti. Tunaomba Watanzania watuelewe na watusamehe kwa sababu tunataka timu hizi zifanikiwe."

"Kwa hiyo wewe Mtanzania ambaye utaweka kimbelembele kwenda kupokea wageni uwanjani wa ndege, kuwasapoti kwa namna yeyote, hatutakuelewa na tutadili na wewe kwa vile ambavyo tunaona inafaa."

"Tumekuwa nchi pekee iliyofanikiwa kuingiza timu mbili mwaka huu, lakini ukishapata mafanikio haupaswi kutumia muda mwingi sana kushangilia hayo mafanikio, unatakiwa uangalie unafanya nini ili kuendelea kupata mafanikio zaidi," alisema

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
6h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
9h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
20h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’