FT : Yanga 5-0 Ihefu Fc

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Mar 2024
FT : Yanga 5-0 Ihefu Fc

Mnara wa 5G umeinuka Azam Complex leo Yanga ikiifumua Ihefu Fc mabao 5-0 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC

Hii ilikuwa mechi ya kisasi na kwa hakika kisasi kimelipwa! Stephane Aziz Ki leo ndiye aliyebeba ramani ya ushindi huo akitoa pasi tatu za mabao huku mwenyewe akifunga pia

Bao la kwanza lilifungwa Pacome Zouzoua katika dakika ya 9 akimalizia pasi ya Aziz Ki

Mudathir Yahya akaweka chuma ya pili katika dakika ya 30 bao likitengenezwa na Aziz Ki

Yanga ikaenda mapumziko ikiwa mbele kwa mabao mawili. Kipindi cha pili Wananchi wakahesabu chuma ya tatu kupitia kwa Aziz Ki dakika ya 68 kabla ya Augustine Okrah kufunga kamba ya nne kwenye dakika ya 84 akimalizia pasi mpenyezo kutoka kwa Aziz Ki

Bao la tano likawekwa kimiani na Maxi Nzengeli katika dakika ya 85, bao ambao hata hiyo ilionekana mshika kibendera hakumsaidia vyema mwamuzi kwani shuti la Nzengeli liligonga mwamba wa juu na kushuka chini lakini picha za marudio zinaonyesha mpira haukuvuka mstari

Ni zile nyakati ambazo waamuzi nao wanafanya makosa kwa kuwa nao ni binadamu. Kama kungekuwa na usaidizi wa VAR, pengine bao hilo lisingehesabiwa

Ni ushindi muhimu kwa Yanga ambao unazidi kuwaimarisha kileleni mwa msimamo wa ligi alama 49 kibindoni

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
5h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
8h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
13h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
17h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’