Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kikosi chake kiko tayari kwa mchezo wa ligi kuu dhidi ya Ihefu Fc ambao utapigwa kesho Jumatatu katika uwanja wa Azam Complex
Gamondi amesema vijana wake wana ari kubwa kuelekea mchezo huo wa kisasi kwani hwajasahau machungu ya kupoteza mchezo wa duru ya kwanza dhidi ya Ihefu Fc
Katika msimu huu, Yanga imedondosha alama tano tu, Ihefu Fc ndio timu pekee iliyofanikiwa kuondoka na alama zote tatu mbele ya Yanga msimu huu
"Kwetu kila mechi ni muhimu na tunataka kushinda hivyo leo tunakwenda kufanya mazoezi ya mwisho ili kuwapa furaha wananchi"
"Tunajua Ihefu ndiyo timu pekee iliyotujeruhi msimu huu na kesho ni siku nzuri ya kulipiza kisasi hiki, wachezaji wanafahamu, benchi la ufundi tunafahamu na tunaamini tutapata alama tatu kesho"
"Binafsi sikufurahi kabisa tulivyocheza mchezo wetu uliopita dhidi ya Ihefu najua pia Wananchi hawakufurahi hivyo nawaomba kesho wajitokeze kwa wingi kwakuwa wachezaji wanatambua kuwa wao ndiyo mchezaji wa 12, waje kwa wingi kushuhudia burudani nzuri na tukipamba kupata alama tatu muhimu," alisema Gamondi
Mchezo huo utapigwa uwanja wa Azam Complex kuanzia saa 12 jioni