Wananchi wamerejea kileleni mwa msimamo wa ligi kibabe baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Namungo Fc katika mchezo uliopigwa uwanja wa Majaliwa
Yanga ilihitaji dakika 45 za kipindi cha pili kuondoka na alama zote tatu wakifunga mabao yao kupitia kwa Mudathir Yahya, Clement Mzize na Stephane Aziz Ki
Bao pekee la Namungo lilikuwa la kujifunga Yanga baada Ibrahim Bacca kujaza mpira wavuni katika harakati za kuokoa
Yanga leo imedhihirisha upana wa kikosi chake kwani licha ya kuwakosa nyota sita wa kikosi cha kwanza, ikitawala mchezo hasa kipindi cha pili
Pengine ushindi ungekuwa mnono zaidi kama Yanga ingetumia vyema nafasi nyingi walizotengeneza
Ni alama 46 kileleni mwa msimamo wa ligi, alama mbili mbele ya Azam Fc inayoshika nafasi ya pili na alama 10 mbele ya Simba inayoshika nafasi ya tatu. Ikumbukwe Yanga bado ina mechi tatu za viporo!