Baada ya mechi za hatua ya makundi ligi ya mabingwa barani Afrika kukamilika jana, kiungo mshambuliaji wa Yanga Pacome Zouzoua ametajwa kuwa mchezaji bora katika hatua ya makundi
Katika mechi sita za makundi, Pacome alihusika katika mabao matano, akifunga mabao matatu na kutoa pasi mbili za mabao. Pacome aliwatungua Al Ahly, akawatungia Medeama nyumbani na ugenini
Amezidiwa bao moja tu na Sankara Karamoko aliyekuwa akiitumikia Asec Mimosas lakini kwa sasa sio mchezaji wa timu hiyo akitimkia barani Ulaya
Hussein El Shahat (Al Ahly) na Abdelraouf Benguit wa CR Belouizdad wamefungana na Pacome wakiwa na mabao matatu
Inaweza kuwa nafasi kwa Pacome kuwania ufungaji bora akihitaji kufunga zaidi katika mechi za robo fainali na hatua zitakazofuata
Mudathiri Yahya nae yuko katika kinyang'anyiro hicho cha ufungaji bora nae akiweka kambani mabao mawili