Kikosi cha Yanga leo kimeanza mawindo ya kuikabili Al Ahly siku ya Ijumaa katika mchezo wa kuhitimisha hatua ya makundi ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Ni mchezo utakaokutanisha timu mbili ambazo tayari zimejihakikishia kucheza robo fainali ya michuano hiyo, hivyo utakuwa mchezo wa kumpata kinara wa kundi
Yanga ilifikia katika Hotel yenye hadhi ya nyota tano, Royal Kempinski ambayo ni mwendo wa takribani dakika 15 kutoka uwanja wa Ndege wa Cairo
Mchezo dhidi ya Al Ahly unatarajiwa kupigwa hapo Cairo ambapo leo Yanga itakuwa na nafasi ya kufanya mazoezi yake ya kwanza katika uwanja utakaotumika IJumaa
Kwa aina ya Hotel ambayo Yanga imefikia, hii inakuonyesha ni kiasi gani Wananchi hawakwenda Misri kutembea, Wananchi wanataka ushindi dhidi ya Al Ahly na kumaliza vinara wa kundi

