Ni mechi ya heshima kwa wachezaji wa Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
24 Feb 2024
Ni mechi ya heshima kwa wachezaji wa Yanga

Achana na mkwanja mrefu ambao wachezaji wa Yanga leo wataondoka nao kama wataibuka na ushindi dhidi ya CR Belouizdad na kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, hii itakuwa mechi ya heshima na kuwatangaza wachezaji

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amefichua kuwa mkwanja uliowekwa mezani na GSM ni zaidi ya kile kitita ambacho wachezaji walichukua baaada ya ushindi wa 5G dhidi ya Simba

Zaidi ya Milioni 500 zitakuwa mikononi kwa wachezaji kama watashinda leo na kufuzu robo fainali

Hii ni mechi ambayo itatizamwa na mashabiki wengi barani Afrika na pengine hata nje ya Afrika

Ni mechi ya wachezaji kutangaza majina yao na kuweka heshima katika uso wa Afrika

Msimu uliopita Yanga ilicheza fainali ya kombe la Shirikisho (CAF CC) na kukosa kombe kikanuni tu, leo ni nafasi nyingine kwa Yanga kuonyesha kwamba tayari iko katika daraja la wale wanaoitwa vigogo

Ni wazi itakuwa mechi ngumu kwa kuwa kila timu inahitaji matokeo ili kujiweka vyema katika vita ya kufuzu robo fainali, lakini hakuna heshima kubwa kama ambayo wataipata wachezaji wa Yanga leo kama watashinda na muhimu kufanikiwa kufuzu robo fainali

Yanga ina dakika 180 za kuwania angalau alama nne ili ifuzu robo fainali lakini inaweza kutumia dakika 90 za leo kufuzu kama itaibuka na ushindi wa kuanzia mabao 4-0

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
10h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
10h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
14h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
14h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
19h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
19h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’