Yanga iko Mbezi, kituo cha Mabasi cha Magufuli kuhitimisha wiki ya hamasa kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CR Belouizdad ambao utapigwa kesho Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Kwa wale Wananchi wa maeneo ya karibu wametakiwa kujitokeza ambapo kutakuwa na burudani mbalimbali pamoja na mashabiki kuweza kukata tiketi
Hadi kufikia asubuhi ya leo zaidi ya nusu ya tiketi tayari zimeshauzwa, hivyo kwa wanaosubiri kununua tiketi dakika za mwisho wanaweza wakakosa kushuhudia Pacome Day 'mbashara'
Matukio mbalimbali ya burudani yanatarajiwa kuanza saa 6 mchana
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe na Mhamasishaji Jimmy Kindoki wataongoza timu ya hamasa
Aidha kutakuwa huduma ya bure ya kupaka 'bleach' kwa Wananchi
ADVERTISE HERE