Baada ya Yanga kukamilika mechi 15 za mzunguuko wa kwanza, kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki anaongoza mbio katika ufungaji bora
Mabao yake 10 aliyofunga katika mechi 12 alizocheza bado yanamfanya aongoze mbio hizo za kuwania kiatu cha dhahabu
Maxi Nzengeli anafuatia akiwa na mabao nane, Pacome Zouzoua akisogea jana baada ya kufunga bao lake la tano katika mchezo dhidi ya Tanzania Prisons
Mudathir Yahya amefunga mabao manne wakati Kennedy Musonda akiwa na mabao matatu, Clement Mzize ana mabao mawili
Yao, Skudu, Hafiz Konkoni na Dickson Job kila mmoja amefunga bao moja kukamilisha idadi ya mabao 36 yaliyofungwa huku wakirwuhusu mabao nane
Aidha Yao ameendelea kuongoza vinara wa mabao jana akiongeza assist ya sita katika mchezo dhidi ya Prisons
Jesus Moloko, Mzize na Pacome Zouzoua kila mmoja ana assist tatu wakati Aziz Ki, Maxi na Nickson Kibabage kila mmoja ana assist mbili
Wachezaji wenye assist moja moja ni Bakari Mwwmnyeto, Konkoni, Mudathir, Musonda, Kibwana Shomari, Job na Khalid Aucho