Yanga imefanikiwa kuondoka na alama zote tatu dimba la Azam Complex wakiichapa Mashujaa Fc mabao 2-1 katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Mudathir Yahya ameipa Yanga alama zote tatu katika mchezo wa pili mfululizo akifunga bao la ushindi katika dakika ya 86
Maxi Nzengeli alifunga bao la uongozi kwa Yanga kwenye dakika ya 45 akimalizia mpira uliotemwa na mlinda lango Erick Johora
Mashujaa walifanya shambulizi lao kubwa la kwanza kwenye dakika ya 65 na wakafunga bao lao kupitia kwa Emmanuel Mtumbuka aliyepiga kombora lililomshinda Aboutwalib Mshery
Lakini mfalme wa Azam Complex, Mudathir akahakikisha alama tatu zinabaki Dar akifunga bao la ushindi akimalizia mpira baada ya krosi ya Kennedy Musonda
Bado Yanga haijarejesha makali yake hasa katika safu ya ushambuliaji kwani ule ukatili ulioonekana kabla ya mapumziko ya Afcon bado kurejea
Ni alama tatu zinazoichimbia Yanga kileleni mwa msimamo baada ya kufikisha alama 37