Konkoni achukizwa na upotoshaji wa Micky Jr

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
4 Feb 2024
Konkoni achukizwa na upotoshaji wa Micky Jr

Juzi mwanahabari kutoka Ghana Micky Jr alisambaza uvumi kwenye kurasa za mitandao ya kijamii akidai kuwa Yanga haikumtendea haki mshambuliaji Hafiz Konkoni

Konkoni amekanusha madai yote yaliyotolewa na Micky huku akisisitiza yeye bado ni mwajiriwa wa Yanga (ametolewa kwa mkopo) na hajawahi kutofautiana na uongozi wa Yanga katika suala la maslahi

"Mimi na uongozi wangu tunasikitika kuhusiana na uvumi unaoendelea kuhusu mimi na Yanga katika wiki za hivi karibuni"

"Nataka kusema kwa msisitizo kwamba, hakujawa na suala lolote la madai ya ada ya usajili au mimi kukataa kuondoka kwa mkopo ikiwa pesa haijalipwa"

"Nimejitolea kikamilifu kwa mwenendo wa klabu na bado niko kwenye mkataba na nimefurahia muda wangu na timu tangu nilipojiunga tangu siku ya kwanza"

"Hadithi zinazoenea kwa muda wa wiki chache ni uwongo mtupu na lazima zipuuzwe kwani mtu yeyote anayesambaza habari kama hizo anasababisha tu mvutano mbaya na hakuna zaidi," aliandika Konkoni kwenye kurasa ya mtandao wake wa kijamii

Mwanahabari huyo kutoka Ghana anafahamika kwa kutoa taarifa zenye mlengo hasi kuhusu klabu ya Yanga

Uongozi wa Yanga umepanga kumchukulia hatua kwa kusambaza taarifa zenye lengo la uchochezi, upotoshaji na kuibua sintofahamu miongoni mwa mashabiki na Wanachama wa Yanga

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’