Alama mbili zimedondoka dimba la Kaitaba baada ya Yanga kulazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa ligi kuu ya NBC
Ulikuwa mchezo ambao Yanga haikutengeneza nafasi ya kutosha, vijana wa Miguel Gamondi hawakuwa katika kasi yao
Kagera Sugar walitumia ipasavyo mbinu ya kupoteza muda, pengine mbinu hiyo iliwasaidia kupunguza kasi ya Yanga kwani kwa wastani mchezo ulisimama kila baada ya mda mchache kwa mchezaji wa Kagera Sugar kuumia
Ni alama moja ugenini, ambayo ni bora kuliko kukosa kabisa



ADVERTISE HERE