Baada ya tetesi za muda mrefu hatimae tunaweza kuthibitisha kuwa mshambuliaji wa Simba Ibrahim Ajib amesaini mkataba wa miaka miwili kuitumikia Yanga.
Wiki yote hii viongozi wa Yanga walikuwa wakihaha kuhakikisha wanaipata sahihi ya mchezaji huyo mwenye kipaji cha hali ya juu.
Kilichokuwa kinawakwamisha ni masharti aliyokuwa ametoa kwa timu hiyo kuwa apatiwe pesa yote ya usajili kiasi cha Mil 50.
Mmoja wa viongozi walio kwenye Kamati ya usajili Yanga ametuthibitishia kuwa Yanga imemalizana na mchezaji huyo leo.
"Tulikuwa hatujamalizana katika masuala fulani ya fedha, lakini sasa naona mambo yamekaa vizuri kabisa. "Kuanzia sasa ukisema Ajibu ni mchezaji wa Yanga tayari, wala hautakosea,""alisema.
Ajib alikuwa mchezaji huru baada ya kumaliza mkataba wa kuitumikia Simba mwishoni mwa mwezi Mei.
Angeweza kujiunga na Singida United ambayo iliweka mezani dau la kiasi cha Tsh Mil 60 na mshahara wa Tsh Mil 3 kwa mwezi lakini Ajib ameangalia zaidi njia sahihi itakayowezesha kutimiza ndoto zake za kucheza soka la kulipwa kwa haraka.
Kwa kuwa Yanga itashiriki michuano ya klabu bingwa barani Afrika msimu ujao ni dhahiri hiyo inaweza kuwa sababu iliyomfanya ajiunge nao.
Simba ilijaribu kumbakisha mchezaji huyo lakini imekiri kushindwa kumshawishi mapema leo uongozi wa klabu hiyo ukidai amepoteza 'morali' ya kucheza Simba.

ADVERTISE HERE