Mwanachama maarufu wa Yanga Jimmy Msindo maarufu 'Jimmy Kindoki' ameongezwa katika Idara ya Wanachama na Mashabiki akiwa Afisa wa Wanachama na Mashabiki
Ni katika mkakati ya kuimarisha Hamasa hasa upande wa Uandikishaji wa Wanachama na Mashabiki
Kindoki amekuwa Mwanafamilia wa Yanga kwa muda mrefu na ameshiriki kikamilifu katika kampeni mbalimbali za hamasa
Sasa ametua kuwaongezea nguvu kina Ali Kamwe yeye akiwa upande wa Wanachama na Mashabiki akitangazwa sambamba na Mwanachama mwingine Khamis Jecha huku Willy Shemoka akiongezwa katika kitengo cha habari
Aidha Yanga imemtangaza Ibrahim Samwel kuwa Mkurugenzi wa Idara ya Masoko, Wanachama na Mashabiki.

ADVERTISE HERE