Michuano ya Afcon 2023 imeanza kutimua vumbi ambapo kwa takribani mwezi mzima, macho na masikio ya wadau wa soka barani Afrika yataelekezwa huko Ivory Coast
Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' iko kundi F na itacheza mechi ya kwanza Januari 17 dhidi ya Morocco
Nyota saba wa Yanga watakuwa katika Mataifa yao katika michuano hiyo
Nahodha Bakari Nondo Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Dickson Job na Mudathir Yahya wao watakuwa sehemu ya kikosi cha Tanzania
Kiungo mshambuliaji Stephane Aziz Ki yuko na Burkina Faso, Djigui Diarra yuko na Mali wakati Kennedy Musonda akiwa na timu ya Taifa ya Zambia
Yanga ni miongoni mwa timu zilizotoa wachezaji wengi katika michuano hiyo mikubwa zaidi ngazi ya timu za Taifa barani Afrika
ADVERTISE HERE