Baada ya kichapo cha aibu cha mabao 3-1 kutoka kwa watani zao Simba Queens, kinadada wa Yanga Princess leo wako uwanjani mkoani Dodoma kuikabili Fountain Gate Princess katika mwendelezo wa Ligi Kuu ya Wanawake
Yanga Princess iliuanza vyema msimu huu kwa kushinda mechi mbili za awali kabla ya kipigo dhidi ya Simba Queens matokeo ambayo yaliwakatisha tamaa wengi
Hata hivyo bado ni mapema ligi ikiwa katika mzunguuko wa nne, Yanga Princess ina nafasi ya kujisahihisha na kurejesha imani ya mashabiki wake ambao wamechoka kuwa wasindikizaji katika ligi kuu ya Wanawake
Mchezo utapigwa katika uwanja wa Jamhuri saa 10 jioni
ADVERTISE HERE