Michuano ya kombe la Mapinduzi inaendelea visiwani Zanzibara ambapo mechi za robo fainali zinaanza kupigwa leo
Mabingwa wa soka Tanzania Bara Yanga wao watachuana na APR katika mchezo wa pili wa robo fainali ambao utapigwa New Amaan Complex, saa 2:15 usiku
Mchezo wa mapema ni kati ya KVZ dhidi ya Mlandege ambao utapigwa saa 10 jioni
Pamoja na kutumia wachezaji wengi ambao sio wa kikosi cha kwanza, Yanga ilifanikiwa kutinga robo fainali ya michuano hiyo kibabe ikiongoza kundi C baada ya kushinda mechi mbili na kutoka sare mchezo mmoja
Hautakuwa mchezo mwepesi kwani APR wana timu imara mchezo wao wa mwisho katika kundi B walitoshana nguvu na Simba
Yanga imepania kushinda mchezo huo ili kutinga nusu fainali na pengine huenda ikakutana tena na watani zao Simba katika hatua inayofuata. Simba kesho watachuana na Jamhuri katika mchezo mwingine wa robo fainali