Gamondi anaamini usajili wa Okrah utalipa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
2 Jan 2024
Gamondi anaamini usajili wa Okrah utalipa

Augustine Okrah ni mali ya Yanga baada ya kutambulishwa rasmi juzi Jumapili usiku wa kuamkia Mwaka Mpya 2024.

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema kiungo huyo atapewa nafasi na anaamini atafanya vizuri

Gamondi amefunguka hayo baada ya utambulisho wa mchezaji huyo, wakati timu yake ikiibuka na ushindi wa kwanza wa mashindano ya Mapinduzi wa mabao 5-0 dhidi ya Jamhuri kwenye Uwanja wa Amaan, Zanzibar.

Okrah ana kazi kubwa ya kufanya kumshawishi Gamondi ambaye mwenyewe alisema uongozi umemfuatilia mchezaji huyo kwa miezi miwili na kubaini ubora wake hivyo anaamini ataisaidia timu hasa kipindi hiki wana mashindano mengi

"Sina wasiwasi na usajili wa Okrah kwa sababu ni mchezaji ambaye ana uzoefu na ligi ya Tanzania na rekodi zake alipotoka kitakwimu ni nzuri, pia uongozi kabla ya kumsajili umemfuatilia Kwa miezi miwili naamini atakuwa msaada kwenye kikosi," alisema.

"Sihitaji kuzungumza mambo mengi sasa kuhusu mchezaji huyo, nitampa nafasi aonyeshe kwa vitendo ubora wake, utakaompa nafasi ya kucheza zaidi, akishindwa kufanya kile tunachokitarajia kutoka kwake atawapisha wengine wacheze," alisema.

Gamondi alisema dirisha hili la usajili ni bahati kupata mchezaji mzuri kutokana na wengi kuwa na mikataba na timu zao na kuivunja ni gharama kubwa.

Okrah aliyewahi kuichezea Simba, ni mchezaji wa pili kusajiliwa na Yanga dirisha hili, baada ya kiungo kutoka JKU, Shekhan Ibrahim Hamis

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
8h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
13h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
13h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’