Hapo uwanja wa Azam Complex sio sehemu salama kucheza na timu yoyote ya Yanga iwe Wanawake, Wanaume na hata U20
Leo Yanga Princess imeibuka na ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Amani Queens katika mchezo wa Ligi Kuu ya Wanawake
Precious Christopher na Janeth Cletus Nyangali walifunga mabao mawili kila mmoja huku Noela na Traole wakipachika bao moja
Ni mwendelezo wa vipigo vinavyotolewa timu za Yanga katika uwanja huo
Yanga Princess inashinda mechi yake ya pili, ikiweka alama sita kibindoni na mabao nane ya kufunga huku ikiwa imeruhusu bao moja tu
Msimu huu Yanga Princess inautaka ubingwa Ligi ya Wanawake



ADVERTISE HERE