Usajili wa Shekhan kama 'movie'

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
14 Dec 2023
Usajili wa Shekhan kama 'movie'

Kiungo wa JKU Shekhan Ibrahim Khamis jana alikamilisha usajili wake kujiunga na Yanga akipewa mkataba wa miaka mitatu na mabingwa hao wa Tanzania Bara

Usajili wake kutua Yanga unaambiwa ulikuwa kama 'movie' kwani kiungo huyo awali alikuwa tayari amefikia makubaliano na Simba na jana alipaswa kutua Dar kwa boti kwa ajili ya kusaini mkataba

Kilichotokea ni kuwa baada ya taarifa hiyo kumfikia Makamu wa Rais wa Yanga Arafat Haji kupitia vyanzo vyake visiwani Zanzibar, haraka 'akapindua meza',akamtumia Shekhan tiketi ya ndege na akatua jijini Dar majira ya mchana

Kiungo huyo mahiri anayetumia mguu wa kushoto, akamalizana na Yanga kisha akakwea pipa kurudi Zanzibar kuweka mambo yake sawa kabla ya kurejea kuanza majukumu ya kuitumikia Yanga baada ya dirisha dogo kufunguliwa

Yanga ilikuwa ya kwanza kuanza mchakato wa kumsajili nyota huyo lakini baadae Simba wakaingilia kati kabla ya Arafat kuwaweka bandarini kwa saa kadhaa hadi waliposikia nyota huyo tayari yuko mitaa ya Twiga na Jangwani

Kipaji cha Shekhan kilianzia kwenye akademi ya JKU kisha msimu huu akapandishwa timu kubwa na kuanza kuchanganya akiwa pia kwenye timu za taifa hilo za taifa chini ya miaka 18.

Kwa mujibu wa kocha wa JKU Msellem Sultan Hemed amesema Shekhan ana kipaji kikubwa na kwamba Yanga imepata mchezaji mdogo bora kwa baadaye

"Huyu naweza kusema atavuma kuliko Fei toto, hawa wote nawajua ni wachezaji bora lakini kitu ambacho Shekhan anazidi ni namna ambavyo ana mudu kucheza nafasi nyingi na kwa uwezo mkubwa, Yanga wamepata mchezaji hasa," alisema Hemed.

Shekhan huenda akawa usajili wa kwanza kutambulishwa na Yanga pale dirisha litakapofunguliwa Disemba 16

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
6h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
7h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
10h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
11h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
15h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
15h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’