Ni mwendo wa rekodi kwa Pacome Ligi ya Mabingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
13 Dec 2023
Ni mwendo wa rekodi kwa Pacome Ligi ya Mabingwa

Mpaka sasa unaweza kusema kiungo mshambuliaji Pacome Zouzoua ndio mchezaji bora wa Yanga katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya mechi tatu za hatua ya makundi

Yanga imepachika mabao mawili katika mechi hizo na yote yamefungwa na Pacome ambaye aliibuka na tuzo ya mchezaji bora wa mwezi (NIC Player of the Month) Novemba 2023

Pacome ameingia mara tatu katika kikosi bora cha wiki cha CAF kwa maana amekuwa mchezaji bora katika kila mechi

Bao lake alilofunga katika mchezo dhidi ya Al Ahly lilikuwa bao bora la wiki la CAF huku bao alilofunga katika mchezo dhidi ya Medeama likitajwa miongoni mwa mabao yanayowania tuzo hiyo katika wiki ya tatu

Katika orodha ya vinara wa kupachika mabao, Pacome anashika nafasi ya pili nyuma ya Sankara Karamoko wa Asec Mimosas aliyefunga mabao matatu

Yanga pia inahusishwa kumuwania Karamoko ambaye msimu uliopita alicheza na Pacome, Yao Kouassi katika kikosi cha Asec

Kwa hakika ni mwanzo mzuri sana kwa Pacome aliyetua katika dirisha la usajili lililopita

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
7h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
11h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
14h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
17h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
1d ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’