Yanga yarejea Avic Town kuiwinda Mtibwa Sugar

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
11 Dec 2023
Yanga yarejea Avic Town kuiwinda Mtibwa Sugar

Baada ya kurejea kutoka Ghana, kikosi cha Yanga leo kimerejea mazoezini Avic Town kujiandaa na mchezo unaofuata ligi kuu ya NBC dhidi ya Mtibwa Sugar

Mchezo huo utapigwa Jumamosi Disemba 16 katika uwanja wa Azam Complex, saa 12:30 jioni

Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi amesema malengo yake ni kuona wanafanya vizuri katika mchezo huo ambao utakuwa sehemu ya maandalizi yao kuelekea mchezo wa raundi ya nne ligi ya mabingwa dhidi ya Medeama ambao utapigwa uwanja wa Benjamin Mkapa, Disemba 20

"Tunarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mtibwa Sugar ambao ndio unaofuata kwa mujibu wa ratiba"

"Kwa sasa tunaelekeza akili zetu katika mchezo huo ili kuhakikisha tunashinda kabla ya kufikiria mechi ya ligi ya mabingwa," alisema Gamondi

Baada ya kikosi chake kutua nchini kutoka Ghana, Gamondi aliwahakikishia Wananchi kuwa bado nafasi kufuzu robo fainali ya ligi ya mabingwa wanayo na watapambana katika mechi tatu zilizobaki

Gamondi alieleza masikitiko yake kwa kikosi chake kukosa ushindi katika mchezo dhidi ya Medeama ambao anaamini walistahili kushinda lakini waamuzi 'waliwabania'

"Bado tuna nafasi jambo zuri pia ni kwamba bado tuna timu imara kupigania malengo yetu, kuna mambo ambayo huwezi kubaki kulalamika unapoona yanatokea, ilikuwa ni safari ambayo kwa haki Yanga ilikuwa inarudi na ushindi lakini haikuwa hivyo kwa makosa ambayo hayapo ndani ya timu yetu"

"Kitu muhimu sasa ni kujipanga vizuri tuna mechi tatu ambazo lazima tubadilishe mambo ili hesabu zizidi kuwa kwetu najivunia wachezaji wangu na hata mashabiki wetu hasa hizi mechi mbili za nyumbani kabla ya kwenda kumalizia ugenini, lazima tujitoea kwa kiwango kikubwa," alisema Gamondi

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
19m ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
3h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
8h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
8h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
12h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’