Usiku wa kuamkia Jumamosi, Disemba 16 2023 dirisha dogo la usajili litafunguliwa na kudumu kwa mwezi mmoja
Hii ni nafasi kwa Yanga kufanya maboresho ya kikosi katika maeneo yenye changamoto
Meneja wa Habari na Mawasiliano wa Yanga Ali Kamwe amesema katika dirisha hilo wataongeza wachezaji kwa kuzingatia mapendekezo ya bench la ufundi
Kamwe amesema tayari usajili wa wachezaji hao umekamilika, dirisha litakapofunguliwa watawatangaza
"Sisi tulianza michakato yetu ya usajili mapema kwa kuzingatia mapendekezo ya benchi la ufundi. Mpaka wakati huu tayari tumekamilisha usajili, dirisha litakapofunguliwa tutawatangaza," alisema Kamwe
Eneo la safu ya ushambuliaji ni miongoni mwa maeneo ambayo yanatarajiwa kuongezewa nguvu
ADVERTISE HERE