Yanga iliondoka Tanzania Alfajiri ya leo Jumanne kuelekea Ghana tayari kwa mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Medeama ambao utapigwa Ijumaa, Disemba 05
Mlinzi wa kushoto Joyce Lomalisa sio miongoni mwa wachezaji walioondoka kwenda kuzisaka alama tatu muhimu huko Ghana
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema Lomalisa alifanyiwa vipimo vya afya jana baada ya kuumia kwenye mchezo uliopita dhidi ya Al Ahly, ameahwa kuendelea na matibabu
"Lomalisa alifanyiwa vipimo vya afya jana kutokana na majeraha aliyopata katika mchezo dhidi ya Al Ahly. Taarifa rasmi kuhusu ukubwa wa jeraha na atakaa nje kwa muda gani itatolewa ingawa daktari amesema hakuumia sana hivyo anaweza kurejea uwanjani mapema"
"Hii ni nafasi adimu kwa Nickson Kibabage kuonyesha kuwa Yanga haikukosea kumsajili kutoka Singida BS," alisema Kamwe
Kikosi kilichoondoka kimejumuisha wachezaji 24, wachezaji watatu wakibaki jijini Dar es salaam ambao ni Crispin Ngushi, Denis Nkane na Joyce Lomalisa
Nyota waliosafiri ni Dickson Job, Nickson Kibabage, Kouassi Yao, Kibwana Shomari, Khalid Aucho, Mudathir Yahya, Salum Abubakar, Pacome Zou-zoua na Jonas Mkude
Wengine ni Zawadi Mauya, Stephane Aziz Ki, Maxi Nzengeli,Β Farid Mussa, Mahlatsi Makudubela na Jesus Moloko
Pia wamo Kennedy Musonda, Clement Mzize, Hafiz Konkoni, Djigui Diarra, Metacha Mnata, Aboutwalib Mshery, Ibrahiim Bacca na Bakari Mwamnyeto