Kundi la pili la wachezaji nane wa Yanga waliokuwa kwenye majukumu ya timu ya taifa (Taifa Stars) limewasili nchini Algeria kujiunga na wachezaji wengine waliotangulia awali tayari kwa maandalizi ya mchezo wa Ijumaa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi CR Belouizdad
Nyota hao watakuwa na muda wa mapumziko kabla ya kuungana na wenzao waliotua Algeria tangu jana
Wachezaji wote waliokuwa na majukumu ya timu za Taifa walitarajiwa kuwasili leo
Yanga itakuwa na siku mbili za mazoezi, muda ambao unatosha kwa maandalizi ya mwisho tayari kuikabili CR Belouizdad Ijumaa, saa 4 usiku
ADVERTISE HERE