Msafara wa pili wa wachezaji wa Yanga waliokuwa na majukumu na timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars', wameondoka nchini Alfajiri ya leo kuelekea Algeria kuungana na wenzao tayari ka mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya CR Belouizdad ambao utapigwa Ijumaa Novemba 24
Jana usiku Stars ilikamilisha mechi ya pili ya kuwania kufuzu kombe la Dunia 2026 kwa kukubali kipigo cha mabao 2-0 dhidi ya Morocco katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Wachezaji waliokuwa Stars ni Metacha Mnata, Aboutwalib Mshery, Nickon Kibabage, Dickon Job, Bakari Mwamnyeto, Ibrahim Bacca, Mudathir Yahya na Clement Mzize
Nyota hao wanatarajia kutua Algeria majira ya saa 12 jioni kwa saa za huko
Aidha Djigui Diarra, Khalid Aucho na Stephane Aziz Ki nao wataungana na wenzao huko Algeria leo