Farid ajipanga kupigania nafasi Yanga

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
15 Nov 2023
Farid ajipanga kupigania nafasi Yanga

Mashabiki wa Yanga wana shauku ya kumuona dimbani kiungo mshambuliaji Farid Mussa ambaye wakati mwingine hutumika kama mlinzi wa kushoto

Msimu haujaanza vyema kwa Farid, majeruhi imekuwa sababu ya kutoonekana kwake uwanjani mara kwa mara. Katika Ligi Farid amecheza mechi moja tu dhidi ya KMC kwa takribani dakika 26

Akiwa amepona majeraha, Farid amesema ana kazi ya kupambana kurejea kikosi cha kwanza kutokana na ushindani uliopo

"Nilikua nje kwa muda kidogo kutokana na majeraha lakini nafurahiu nimepona na nimerejea kuipambania timu yangu"

"Natambua ugumu wa kupata nafasi kutokana na ubora wa kikosi lakini sijakata tamaa nitapambana kuhakikisha napata nafasi ya kucheza ili kuwa miongoni mwa wachezaji ambao wameipa mafanikio timu japo sio rahisi lakini inawezekana"

"Mimi nacheza nafasi nyingi uwanjani lakini ukiangalia zote zina watu wazuri na wote wana mchango mkubwa kwenye timu kazi kwangu kuhakikisha napambana ili kupata nafasi," alisema Farid

Mabadiliko ya mfumo wa uchezaji yaliyofanywa na kocha Miguel Gamondi huenda yakawa yamechangia kupunguza nafasi kwa baadhi ya wachezaji akiwemo Farid

Kwa sasa Yanga haitumii mawinga asilia, viungo washambuliaji watatu (Maxi, Aziz Ki na Pacome) wakitumika

Upande wa safu ya ulinzi wa kushoto Mcongomani Joyce Lomalisa amekuwa na msimu bora na hivyo sio rahisi kwa Gamondi kumuweka nje anapokuwa yuko 'fit'

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
4h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
7h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
12h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
12h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
16h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’