Mapema leo Yanga iliweka hadharani bango la '5G' ambalo limewekwa barabara ya Ali Hassan Mwinyi. Kuna baadhi walichukulia kama ni bango tu na kuwa klabu inapoteza fedha kwa kufanya jambo hilo pasipo kujua faida ya kibiashara iliyojificha ndani ya ubunifu huo wa Wananchi
Mkurugenzi wa Sheria wa Yanga Simon Patrick ametoa ufafanuzi ambapo amesema jambo kubwa la kwanza lililofanywa na Yanga kupitia bango hilo ni kutambua thamani ya Wadhamini wao na hivyo kufungua mlango wa fursa kwa Wadhamini zaidi kujitokeza kuweka fedha zao Yanga
Aidha bango hilo pia limedhaminiwa, SAIFI STORE wameweka fedha kwa bango hilo kuonekana huku nafasi ikitolewa kwa Wananchi kupiga picha na bango kisha kujipatia jezi zilizosainiwa na wachezaji
"Wakati watu wengi wanaona 5G kwenye bango, sisi tunatambua mchango na thamani ya wadhamini wetu ambao ni @tzsportpesa @gsmgroupofcompanies @haiertanzania @azamtvtz na @nic_insurance"
"Wadhamini hawa wameendelea kuifanya Yanga itambe na kusimika mimara ya 5G toka ligi ianze, tunatumia fursa hii kuwaalika wadhamini wengine ambao wangependa kudhamini 5G zinazokuja ndo muda sasa wa kuchangamkia fursa"
"Tuendelee kupiga picha kwenye bando, kisha kuzipost huku ukiutag ukurasa rasmi wa @yangasc ili ujishindie zawadi nono," aliandika Simon kwenye ukurasa wake wa mtandao wa kijamii