Yanga iliandika historia msimu uliopita kwa kucheza fainali ya michuano ya kombe la Shirikisho (CAF CC) Wananchi wakikosa ubingwa kwa kanuni ya bao la ugenini baada ya sare ya mabao 2-2 dhidi ya USM Alger katika mechi mbili za fainali
Ni wazi Kocha Mkuu wa Yanga Miguel Gamondi ana kazi ya kuhakikisha anaendeleza pale alipoishia Nasreddine Nabi katika michuano ya CAF CL
Jukumu lake la kwanza ni kuhakikisha anaipeleka Yanga hatua ya robo fainali. Yanga imesubiri miaka 25 kucheza hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa lakini Gamondi alimaliza ukame huo
Gamondi anafahamu ukubwa wa jukumu lililo mbele yake kwani amewahi kuwa sehemu ya benchi la ufundi la timu kama Wydad Athletic ambao karibu kila msimu wanavuka hatua ya robo fainali
Kocha huyo raia wa Argentina ameonyesha kuwa na imani kubwa na kikosi chake akibainisha kuwa kama wachezaji watajituma na kuendeleza ubora walionao sasa, basi msimu huu Yanga itafanya vizuri kwenye michuano ya Ligi ya Mabingwa
Kibarua chake cha kwanza kundi D kitakuwa ugenini Novemba 24 huko Algeria dhidi ya timu aliyowahi kuifundisha CR Beluizdad
Baada ya mchezo huo Disemba 02 Yanga itacheza mechi yake ya kwanza nyumbani dhidi ya Al Ahly