Kituo kinachofuata ni Ligi ya Mabingwa

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
9 Nov 2023
Kituo kinachofuata ni Ligi ya Mabingwa

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union jana katika mchezo wa ligi kuu ya NBC, Yanga inarejea Dar kuanza mawindo ya hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa barani Afrika

Kutakuwa na mapumziko ya takribani wiki mbili kupisha mechi za Kimataifa zilizo kwenye kalenda ya FIFA na baada ya mapumziko hayo, mechi za hatua ya makundi ya Ligi ya mabingwa zitaanza

Yanga ambayo iko kundi D, itaanzia ugenini nchini Algeria Novemba 25 kwa mchezo dhidi ya Mabingwa wa Algeria CR Belouizdad

Baada ya mchezo huo Yanga itarejea jijini Dar es salaam kuumana na mabingwa watetezi Ligi ya Mabingwa Al Ahy, mchezo ukipigwa Disemba 02 katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Ni bandika bandua, kwani baada ya mchezo huo Yanga itasafiri nchini Ghana kuwakabili mabingwa wa Ghana, Medeana Fc katika mchezo raundi ya tatu hatua ya makundi

Disemba 16 Yanga itarejea kwenye mikiki mikiki ya Ligi Kuu kwa mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar ambao utapigwa uwanja wa Azam Complex kabla ya kurudiana na Medeama Disemba 20

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
Hersi atembelea Makao Makuu ya Al Ahly
9h ago
READ MORE β†’
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
Mashabiki Club Africain bado hawajaisahau Yanga
13h ago
READ MORE β†’
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
Ni Gusa Achia Twende Kwao?
18h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
Aziz Ki atunukiwa tuzo ya kukuza vipaji
18h ago
READ MORE β†’
Baada ya Manqoba nani anafuata?
Baada ya Manqoba nani anafuata?
18h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
Magazeti ya leo Alhamisi, Oktoba 29 2026
22h ago
READ MORE β†’
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
1d ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
1d ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’