Hersi, Arafat wapewe maua yao

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
7 Nov 2023
Hersi, Arafat wapewe maua yao

Wakati Rais wa Yanga Injinia Hersi Said anaingia madarakani pamoja na mwenzake Makamu wa Rais Arafat Haji kuna propaganda ziliendeshwa sana mitandaoni kuwa 'watoto' hawa hawawezi kuifanyia Yanga makubwa

Lakini wakiwa katika mwaka wa pili wa uongozi wao, kila kitu kimebaki historia, Yanga imetwaa mataji yote ya ndani katika misimu miwili iliyopita pamoja na kucheza fainali ya kombe la Shirikisho barani Afrika

Yanga sasa inashika nafasi ya 18 katika viwango vya ubora wa CAF kutoka nafasi ya 75 ndani ya miaka miwili tu

Ni hivi karibuni CAF wameitaja Yanga kuwa moja ya klabu 10 zinazowania tuzo ya klabu bora ya mwaka 2023 barani Afrika

Mabadiliko ya mfumo wa uendeshaji wa klabu yameongeza Wadhamini na sasa Yanga inaweza kuwa klabu inayoongoza kwa kuingiza mapato kutoka kwa wadhamini katika ligi kuu ya NBC

Sasa Yanga imefikisha zaidi ya Wanachama 79,000 katika miaka miwili ya Mabadiliko malengo yakiwa kufikisha Wanachama 100,000

Tumeshuhudia maboresho katika benchi la ufundi na wachezaji, leo hii mashabiki wa Yanga wana kila sababu ya kutamba kwani wana kikosi bora pamoja na benchi bora la ufundi chini ya Kocha Miguel Gamondi

Katika kizazi cha vijana wa sasa hakuna aliyewahi kushuhudia Yanga ikipata ushindi wa mabao matano dhidi ya Simba, juzi vijana wa kizazi pipya wameshuhudia!

Ilikuwa imepita miaka 55 tangu Yanga iliposhinda mabao matano au zaidi katika mchezo wa dabi dhidi ya Simba

Ni ushindi wa kihistoria ambao Yanga waliupata mbele ya Simba iliyotimia! Mara nyingi Yanga ilipoteza mechi dhidi ya Simba kwa idadi kubwa ya mabao ikiwa kwenye migogoro

Kwa hakika huu ndio wakati bora zaidi wa mafanikio kwa Yanga katika miaka 88 tangu klabu ilipoundwa

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
3h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
3h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
13h ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
14h ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
16h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
21h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1d ago
READ MORE β†’