Mohammed Ibrahim 'Mo' aje asije?

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
26 Mar 2018
Mohammed Ibrahim 'Mo' aje asije?
Wakati msimu ukielekea ukingoni, tayari harakati za usajili kwa ajili ya msimu ujao zimeanza ambapo timu zimeanza kuweka sawa mambo.

Kiungo mshambuliaji wa Simba Mohammed Ibrahim 'Mo' ni miongoni mwa wachezaji ambao wameweka bayana mustakabali wao kuelekea msimu ujao.

Mo ameuambia mtandao wa GOAL kuwa msimu ujao hatakuwa mchezaji wa Simba na kwa kuwa mkataba wake unamalizika Juni, tayari ameshaweka sawa masuala yake ya usajili.

Kuna taarifa kwamba Mo atakuwa miongoni mwa maingizo mapya kwenye kikosi cha Yanga msimu ujao.

Tangu kuwasili kwa kocha Pierre Lechantre, Mo hajawahi kupata nafasi kwenye kikosi cha Simba. Hivi karibuni alisimamishwa na klabu hiyo ikielezwa kuwa na matatizo ya utovu wa nidhamu.

Kuna wakati alikacha mazoezi kwenye kikosi cha Simba baada ya kuchukizwa na hali hiyo ya kutopewa nafasi na benchi la Ufundi.

Yanga bado inasaka mshambuliaji wa pembeni mwenye kasi kwani tangu kuondokwa Simon Msuva, haijafanikiwa kuziba pengo lake.
ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
Kundi la Yanga kama msimu uliopita tu
13h ago
READ MORE β†’
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
Yanga yatupwa kundi B CAFCL
13h ago
READ MORE β†’
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
Mzize ndio ameanza msimu hivyo
17h ago
READ MORE β†’
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
Timu zinazoweza kukutana na Yanga makundi CAFCL
17h ago
READ MORE β†’
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
Dladla alia na umaliziaji Yanga licha ya ushindi dhidi ya Mashujaa FC
21h ago
READ MORE β†’
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Highlights: Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
22h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
Magazeti ya leo Jumatano, Oktoba 28 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
1d ago
READ MORE β†’