Uongozi wa klabu ya Yanga umewasilisha malalamiko kwa Bodi ya Ligi kufuatia kitendo cha shabiki wake kushambuliwa na mashabiki wa Simba uwanja wa Benjamin Mkapa katika mchezo wa ligi kuu ya NBC kati ya Simba dhidi ya Ihefu
Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe amesema pamoja na kuwasilisha malalamiko hayo kwa mamlaka husika, amesisitiza mashabiki wa Yanga na Simba kuwa waungwana kwani wao ni watani na sio maadui
Aidha Kamwe amewataka wasemaji wa klabu zote kufanya kazi zao kwa kuzingatia weledi wajiepushe kutumia kauli za uchochezi ambazo zinaweza kusababisha maafa
"Hivi karibuni tumemsikia msemaji wa Simba akitoa kauli sisi na wao sio watani tena, nafikiri maafisa wa habari tuna wajibu mkubwa na tunapaswa kujiepusha kutumia kauli ambazo zinaweza kuwachochea mashabiki kufanya matukio ambayo sio ya kiungwana"
"Yanga na Simba ni watani wa jadi, sisi utani huu tumeukuta na tutauacha. Tutaniane, tuzomeane kama sehemu ya utamaduni wetu lakini nje ya mpira sisi ni ndugu na hatupaswi kupigana," alisema Kamwe