Kiungo mshambuliaji wa Yanga Maxi Nzengeli amesema jukumu lao kama wachezaji ni kuhakikisha wanawapa furaha mashabiki wao kwa kuibuka na ushindi katika kila mchezo
Nzengeli amesema mashabiki wa Yanga wana ukaribu na timu yao na hilo limewafanya wachezaji kujihisi kama wana deni wanapokuwa uwanjani
Ijumaa iliyopita Maxi aliiongoza Yanga kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida BS katika mchezo wa ligi kuu ambao ulipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Maxi alifunga mabao yote na sasa akifikisha mabao matano msimu huu akiwa nafasi ya tatu kwenye orodha ya vinara wa mabao nyumba na Stephane Aziz Ki na Jean Baleke ambao kila mmoja ana mabao sita
"Ninafurahi kwa sapoti kubwa tunayopata kutoka kwa mashabiki wa Yanga. Jambo muhimu ni kuhakikisha tunawapa furaha kwa kushinda kila mchezo. Nafurahi nikiifungia timu yangu jambo muhimu zaidi ni ushindi na kuongeza pointi tatu"
"Sisi wachezaji tutaendelea kupambana kwa ajili ya timu yetu ili tuweze kutimiza malengo na kuwapa furaha mashabiki wetu," alisema Maxi
Katika mechi saba za ligi kuu msimu huu, Maxi amehusika kwenye mabao saba, akifunga mabao matano na kutoa assist mbili
Kituo kinachofuata ni dhidi ya Simba, Jumapili Novemba 05