Mchezaji bora wa mwezi Yanga kuvuna Tsh Milioni 4

Shabiki NambaMoja By Shabiki NambaMoja
β€’
28 Oct 2023
Mchezaji bora wa mwezi Yanga kuvuna Tsh Milioni 4

Klabu ya Yanga kwa kushirikiana na Wadhamini Shirika la Bima la Taifa (NIC) wametangaza mchakato wa utolewaji wa tuzo ya mchezaji bora wa Yanga kwa mwezi Oktoba 2023

Meneja wa Habari na Mawasiliano klabu ya Yanga Ali Kamwe ametaja majina ya wachezaji watatu ambao watapigiwa kura na mshindi kutangazwa siku ya Jumanne

Stephane Aziz Ki, Maxi Nzengeli na Dickson Job ndio wachezaji wanaochuana kuwania tuzo ya Oktoba ambapo mshindi ataondoka na kitita chs Tsh Milioni 4. Kura zitapigwa kupitia App rasmi ya klabu ya Yanga

Kamwe amesema mchakato wa kuwapata wachezaji hao ulizingatia tathmini ya kiwango alichoonyesha kila mchezaji katika mwezi husika

"Baada ya kuingia mkataba na NIC, uongozi wa Yanga uliunda Kamati maalum ya kufanya Tathmini ya mechi zote za mwezi husika na kutupatia majina matatu ya wachezaji watakaowania tuzo ya mchezaji bora kisha sisi tumeyaleta kwa Wananchi kwa ajili ya kupigiwa kura," alisema Kamwe

Mshindi pia atakabidhiwa tuzo ya kumtambua kama mchezaji bora wa mwezi husika ambayo itatolewa na Wadhamini NIC

ADVERTISE HERE

Yanga SC Stories

Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
Magoli; Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL (FT)
5m ago
READ MORE β†’
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
FT : Yanga 2-1 Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
30m ago
READ MORE β†’
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Kikosi : Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
3h ago
READ MORE β†’
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
Yao bado kidogo, Diarra tayari kurejea
8h ago
READ MORE β†’
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
Matchday; Yanga vs Mashujaa Fc, NBC PL, Oct 27
11h ago
READ MORE β†’
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
Yanga inahitaji utulivu, si vita ya lawama
12h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
14h ago
READ MORE β†’
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
Maandalizi ya kuikabili Mashujaa Fc yamekamilika
23h ago
READ MORE β†’
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
Aziz Ki amemaliza adhabu, tayari kurejea kikosini
1d ago
READ MORE β†’
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
Tunajua tumewaumiza, tuko tayari kupambana - Dladla
1d ago
READ MORE β†’